Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada ulishiriki Maonesho ya Utalii na Usafirishaji yaliyofanyika jijini Monatreal, Canada tarehe 25 hadi 27 Oktoba, 2019. Taasiri za Serikali kutoka Tanzania nazo zilishiriki zikiwemo  Bodi ya Utalii Tanzania  (TTB), Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Mamlaka za Hifadhi za Taifa (TANAPA)..